Baada ya TCRA Kumtaka Uwoya Aombe Radhi kwa Picha ya Utupu..... Hatimaye Aomba Radhi Kwa Picha kwa Kutumia Picha Tata

Mwandada muigizaji wa filamu za kibongo Irene Uwoya leo aliitwa na Tcra baada ya picha yake ya utupu ile iliyoleta gumzo mtandaoni na kutakiwa kuomba radhi kupitia mtandao wake wa kijamii.

Baada ya kuonywa na TCRA Uwoya alitekeleza agizo hilo alilopewa kwa kutumia picha nyingine tata ilioonyesha mapaja yake wazi  na kuomba msamaha kama alivyotakiwa .

Kupitia instagramu yake irene uwoya aliandika hivi "Wapenzi Wangu ...ndugu zangu...wakubwa zangu na wadogo zangu naomba radhi kwapicha niliyopost...najua niliwakwaza mnisamehe sana sikujua ntawakwaza nisababu tu ya role model Wangu beyonce!!!nimejifunza Sasa!!!nawapenda"


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad