Baada ya Yanga Kunusurika Kukimbiwa na Yondani Hichi Ndicho Wameamua Sasa

Hatimaye uongozi wa klabu ya Yanga umekata mzizi wa fitina kwa kumalizana na mchezaji wake, beki Kelvin Yondani kwa kusaini naye mkataba wa miaka miwili.

Hatua hiyo imefikiwa mwafaka mara baada ya mazungumzo mrefu baina ya uongozi na Yondani kumalizana vizuri.

Mkataba huo amesaini zikiwa zimesalia saa kadhaa dirisha la usajili nchini kufungwa wakati hapo awali alikuwa anatajwa kutua Simba.

Licha ya tetesi za beki huyo kuelezwa anawindwa na Simba, Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara aliibuka na kukanusha vikali kauli hiyo akisema hakuna ukweli wowote juu ya Yondani kuhitajika Simba.

Beki huyo sasa atasalia Yanga mpaka mwaka 2020 baada ya kutia kandarasi hiyo ya miaka miwili kuendelea kukipiga na Yanga
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad