Baba wa Obi Mikel amlaumu mwanaye

Baba wa Obi Mikel amlaumu mwanaye
Kufuatia tukio la kutekwa lililotokea hivi karibuni, baba wa nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria, Obi Mikel amezungumzia mahusiano yaliyopo kwa sasa kati yake na mwanaye huku akimlaumu kwa kutompigia simu.

Michael Obi (74) ambaye alitekwa mwezi uliopita alipokuwa njiani kutoka mjini Jos kuelekea katika kikao cha familia kwenye mji mwingine amesema kuwa hilo halikuwa tukio la kwanza kwake kutekwa, akitaja kuwa mara ya kwanza ilikuwa Agosti 2011.

Obi Mikel alipata taarifa za kutekwa baba yake masaa machache kabla ya mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wa kombe la Dunia dhidi ya Argentina lakini aliuficha uongozi juu ya suala hilo ili aweze kucheza .

Michael Obi alipoulizwa ni kwanini mwanaye alikubali kucheza mchezo huo licha ya kupata taarifa za kutekwa kwake akasema kuwa mawasiliano kati yake na mwanaye si mazuri.

“ Mawasiliano yangu na Obi Mikel ni tatizo, lakini wote hatujui cha kufanya. Ni miaka mitano sasa hajawahi nipigia simu licha ya kuwa huwa anawasiliana sana na mama yake “. Amesema Michael Obi.

“ Sina cha kufanya kwa sasa kuweza kumaliza tatizo hilo, Mungu ameniambia kwamba sipaswi kujiskia vibaya na kuhusu kuongea na yeye kwangu ni sawa tu ilimradi ninamwona katika TV akifanya makubwa “, Ameongeza .
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad