Baada ya kuachana kwa muda mrefu na kila mtu kujiingiza katika mahusiano mapya yaliyosababisha kila mmoja kuendelea na maisha yake , hivi karibuni Barnaba classic alimtupia kijembe mama watoto wake anaejulikana kwa jina la Zuu mela kwa kumwambai kuwa anamuona kama amezeeka kwa sasa.
Nini tasfiri ya Barnaba kwa mama watoto wake, ni kwamba Barnaba anaona kama Zuu alikuwa akionekana kijana kipindi wako nae ila kwa sasa kwa sababu yuko nje ya mahusiano yao anaona kama ameshaanza kuzeka kitu ambacho pia zuu aliamua kumjibu na kumwambia inawezekana ametumwa.
Katika picha ya mwanadada huyo barnaba aliandika
“Macho yangu au laaha, naona unazeeka mama watoto?’ Zuu nae aliamua kumjibu katika uwanja huo wa maoni na kumjibu “utakuwa umetumwa wewe sio bure kabisa, wakati moyoni unasema zuu kawa mcharo.”
Wawili hao waliishi kwa muda mrefu na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kike lakini penzi lao lilikuja kuyeyuka bila kuweka wazi chanzo cha mahusiano hayo kufa.