Brazil Yaondolewa Kombe la Dunia kwa Kufungwa 2-1

Brazil Yaondolewa Kombe la Dunia kwa Kufungwa 2-1
USIKU wa  leo Ubelgiji imewashangza wadau wengi wa soka baada ya kutinga nusu fanali ya michuano ya Kombe la Dunia kwa kuiondosha Brazil kwa kuifunga mabao 2-1.


Ubelgiji ambayo ilikuwa haipewi nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo, ilifanya maajabu hayo kwenye Uwanja wa Kazan mjini Moscow nchini Urusi. Kutokana na ushind huo, sasa Ubelgiji itakutana na Ufaransa waliowaondosha Uruguay kwa mabao 2-0 katika mchezo wa mapema wa robo fainali.


Mchezo wao wa nusu fainali utapigwa Julai 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa St Petersburg. Mchezo kati ya Brazil na Ubelgiji ulianza kwa kila timu kumvizia mwenzake, lakini walikuwa Ubelgiji walioandika bao la kwanza kupitia kwa beki Mbrazili, Fernandinho aliyejifunga dakika ya 13 wakati akiwa katika harakati za kuokoa mpira wa kona.




Baada ya bao hilo kuingia, Brazil walikuja juu na kusaka bao la kusawazisha, lakini walijikuta wakipata tabu sana baada ya kufungwa la pili dakika ya 31 kupitia kwa staa wa Klabu ya Manchester City, Kevin de Bruyne kwa shuti kali akiwa nje kidogo ya 18 baada ya kupokea pasi murua kutoka kwa straika, Romelu Lukaku aliyewachekecha walinzi wa timu pinzani.



Bao hilo ni kama liliwaamsha usingizini Brazil kwani walipeleka mashambulizi makali langoni mwa Ubelgiji lakini umakini mdogo wa wachezaji wake kama Neymar, Phillipe Coutinho na wengineo
ulisababisha wajikute wanamaliza kipindi cha kwanza wakiwa nyuma kwa mabao 2-0.


Kocha wa Brazil, Tite alifanya mabadiliko kadhaa kikosini mwake ikiwemo ya kumtoa Willian na nafasi yake ikachukuliwa na Firmino, huku Renato Augusto akiingia badala ya Paulinho. Baada ya mabadiliko hayo, Brazil walikuja juu na kufanikiwa kupata bao la kwanza kupitia kwa Augusto dakika ya 76 akiunganisha kwa kichwa krosi iliyochongwa na Coutinho ambaye alikosa mabao mengi jana usiku.

Brazil itabidi wajilaumu wenyewe kwani walikosa mabao mengi ya wazi na kama wangekuwa makini basi wangepata ushindi mkubwa katika mchezo huo. Ubelgiji sasa itapambana na Ufaransa Julai 10 katika mchezo wa nusu fainali na mara ya mwisho timu hizo zilikutana mwaka 2015 katika mchezo wa kirafi ki ambapo Ubelgiji ilishinda mabao 4-3. Mafanikio ya mwisho kwa Ufaransa kwenye Kombe la Dunia ni kumaliza nafasi ya pili mwaka 2006 na Ubelgiji ni kutinga hatua ya robo fainali mwaka 2014.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad