Breaking: Julias Mtatiro Akamatwa na Polisi kwa Tuhuma za Kumkashifu JPM

Julias Mtatiro Akamatwa na Polisi kwa Tuhuma za Kumkashifu JPM
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) anashikiliwa na Polisi katika kituo Kikuu cha Polisi tangu jana Julai 5, 2018. Anatuhumiwa kwa kusambaza ujumbe uliomkashfu Rais Magufuli kupitia ukurasa wake wa Facebook uliosema “Rais kitu gani bwana?”



=========================

MWENYEKITI WA KAMATI YA UONGOZI CUF TAIFA MHE. JULIUS MTATIRO YUPO NGANGARI;

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA

Imetolewa leo Tarehe 5 July,2018
Na. Kurugenzi ya Habari –CUF Taifa

Jana Tarehe 4/7/2018 Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa Mhe. Julius Mtatiro alipokea simu ya wito wa kuhitajika kituo Cha Polisi (Central Police) Dar es Salaam.

Leo Tarehe 5/7/2018 Mhe. Julius alikuwa amealikwa kama Mmoja wa Wageni wawezeshaji wa mjadala na Taasisi ya Twaweza katika Kongamano la kujadili MAONI YA WANANCHI KUHUSU USHIRIKI, MAANDAMANO NA SIASA lillilopangwa kufanyika katika kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere International Convention Centre –JNICC. Ilipofika saa 3 asubuhi akiwa anaelekea huko alipigiwa simu kujulishwa afike kituoni hapo saa 4 asubuhi.

Niliambatana nae (Maharagande) mpaka kituoni hapo na tulipokelewa na ZCO na kujulishwa kuwa anahitajika achukuliwe maelezo yake kuhusu ujumbe aliotuma katika ukurasa wake wa facebook unaosema “RAIS KITU GANI BWANA”. Tukakabidhiwa Maafisa wa Polisi wa kufanya kazi hiyo. Wakati wa kuanza kuchukuliwa maelezo yake alielezwa kuwa anatuhumiwa kwa “ KUTUMA UJUMBE WA KUJELI NA KASHFA DHIDI YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA” kupitia mtandao wa kijamii. Mhe Julius amechukuliwa maelezo yake mpaka saa 10 jioni na baadae kuelekea nyumbani kwake kwa upekuzi na kurejea tena kituoni majira ya saa 4 usiku. Maafisa wa polisi wameeleza kuwa wataendelea kuwa nae mpaka kesho asubuhi na kutujulisha kama watampatia dhamana au vinginevyo.

KUHUSU SHAURI LA RITA NA. 13/2018:

Litaendelea kesho Tarehe 6/7/2018 muda wa saa 4 asubuhi baada ya wakili wa Lipumba Mashaka Ngole kudai kuwa hajisikii vizuri (anaumwa) hataweza kwa leo kumfanyia Cross Examination Shahidi wa Pili katika shauri hili Mhe. Joran Bashange [Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Tanzania Bara, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Fedha na Uchumi na katibu wa Bodi ya Wadhamini ya CUF]

Mwisho:

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi Taifa Mhe. Julius mtatiro anawataka wanachama wa CUF kujitokeza kwa wingi Mahakamani kushuhudia Hoja makini zitakazotolewa na Mheshimiwa Bashange. Na wala wasiwe na hofu yeyote juu yake kwani yupo NGANGARI SANA. Shukrani kwa Msomi Wakili Hashimu Mziray kwa kusimamia vyema mahojiano hayo, Bakari Kasubi –Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mzimuni, Shaweji Mketo-Naibu Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF Taifa, Anderson Ndambo na Kassimu Chogamawano[maafisa wa Kurugenzi ya Habari Taifa] kwa Uratibu wenu wa suala hili mpaka saa 5 za usiku huu.

HAKIKA TUPO VIZURI SANA, MAPAMBANO YA KISHERIA YANAENDELEA NA HAKI ITASHINDA.

HAKI SAWA KWA WOTE

____________________
MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI
NA MAHUSIANO NA UMMA-TAIFA.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad