Breaking News: Mbunge wa Monduli Kupitia Chadema Ajiuzulu Ubunge na Kujiunga na CCM


ARUSHA: Aliyekuwa Mbunge wa Monduli kupitia CHADEMA, Julius Kalanga amejiuzulu nafasi hiyo na kujiunga na CCM kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi Rais Magufuli

Kalanga amejiunga jana usiku Julai 30 na kupokelewa na Katibu Mwenezi na Itikadi wa CCM, Humphrey Polepole

Amesema kuwa siasa za uhasama, malumbano na chuki zimemuondoa CHADEMA na kuamua kuunga mkono Serikali ya awamu ya 5 kwa maslahi ya taifa kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili bila kuonekana msaliti

Aidha, amewaomba msamaha Wana-Monduli na kuwaomba wamuelewe na ataenda kuzungumza nao siku si nyingi

Ikumbukwe kuwa Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia CHADEMA 2015
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad