Breaking News: Pigo Kubwa CHADEMA, Mbunge Wake Jimbo la Ukonga Mwita Waitara Atangaza Kuhamia CCM


Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara amejiuzulu uanachama wa chama hicho na kujiunga na CCM leo Jumamosi Julai 28, 2018.


Waitara ametangaza uamuzi wake huo leo katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika ofisi ndogo za CCM Lumumba mjini hapa, akiwa sambamba na katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho, Humphrey Polepole.


Kwa uamuzi huo wa Waitara ambaye alikuwa CCM kabla ya kujiunga Chadema, jimbo la Ukonga linabaki wazi.


Waitara amekuwa mbunge wa pili wa Chadema na wa tatu wa upinzani kuhama chama na kujiunga na CCM. Wengine wa Dk Godwin Mollel (Siha) na Maulid Mtulia (Kinondoni).
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad