Rais Magufuli ametangaza hayo Jumamosi hii katika mabadiliko ya wakuu wa Mikoa na Wilaya ambapo pia amewateua Mosese Machali kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu na Patrobas Katambi ambaye amewahi kuiwa Mwenyekiti wa BAVICHA kabla ya kuamia CCM kuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma.
Pia Rais Magufuli amemteuwa Daniel Godfrey Chongolo kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni na na Ally Hapi ambaye alikuwa akikalia kiti hicho amekuwa mkuu wa Mkoa wa Iringa.
Naye David Kafulila ameteuliwa kuwa Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.