Casto Awatolea Povu Wanaomtukana Mtandaoni Kuhusu Mwanaye "Nikiposti Picha ya Mwanangu Nikaandika Get Well Soon Aisaidii Lolote"

Casto Awatolea Povu Wanaomtukana Mtandaoni Kuhusu Mwanaye "Nikiposti Picha ya Mwanangu Nikaandika Get Well Soon Aisaidii Lolote"
Baada ya Instagram kuchafuka na Casto Dickson kupewa lawama kuhusu mtoto wake Kuumwa, na yeye kuonekana anaposti picha akiwa anakula bata na  mpenzi wake Tunda bila kupost mwanaye na kuonyesha isia zake juu ya mwanaye

Casto afunguka kinachoendelea kati yake na Muna Love kuhusu issue hiyo wakati akifanyiwa interview na clouds.

"Najua watu wengi wameshtuka kuona napost show inayofanyika jumapili  huku mwanangu anaumwa imeniuma ila mimi sijui lolote kuhusu hali ya mtoto kwakuwa mimi nimepata taarifa kutoka kwa bibi yake kuwa mtoto anaumwa tena washampeleka Nairobi simlaumu ila nimempigia Muna mara Tatu ajanipokelea" Casto.

"Nimetukanwa sana instagram pia najua kuna watu wengi wamenichukia kuhusiana na hali ya mwanangu ila hata nikiposti picha ya mwanangu nikaandika get well soon aisaidii lolote nimekaa kimya real love ipo moyoni mwangu na mimi ndio ninayejua mapenzi ya mwanangu ila nimechukia sana kwakuwa m9imi siwezi kupata taarifa za mwanangu kupitia instagram" alisema.

Kasto amesema mwanaye anasumbuliwa na maumivu makali ya kichwa na kuwataka watanzania wasimuone kuwa yeye si baba bora kwakuwa bado anamapenzi mwanaye ila taarifa za mwanaye zinachelewa kumfikia kutokana na mahusiano mabaya aliyonayo kati ya yeye na mzazi mwenzake.

Top Post Ad

Below Post Ad