Chama cha Mapinduzi (CCM), kimefunguka na kumjia juu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe kwamba sio kweli wamezuiliwa kufanya mikutano ya hadhra katika majimbo yao kama wasemavyo bali wao wenyewe ndio hawataki kufanya.
Hayo yamebainishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa (CCM), Humphrey Polepole kwenye mjadala wa uzinduzi wa ripoti ya pili Twaweza kuhusiana na hali ya siasa nchini uliofanyika Julai 05, 2018 na kusema hakuna chama chochote kilichokatazwa kufanya mikutano ya hiyo.
"Mikutano ya hadhara haijapigwa marufuku ila imewekewa utaratibu mzuri zaidi wa namna ambavyo tunapaswa kufanya siasa katika nchi yetu. Tatizo lililokuwepo katika mikutano ya hadhra haifanyiki na wanaoongoza kutofanya hivyo sio CCM bali ni upinzani, na hawafanyi kwasababu hawaishi katika majimbo yao husika ambayo wamepigiwa kura na wananchi wao", amesema Polepole.
Pamoja na hayo, Polepole ameendelea kwa kusema "kwa mfano Mh. Mbowe tangu alipochaguliwa mwaka 2015 mkutano wake wa kwanza ameufanya Hai mwaka 2017 lakini yeye na chama chake wamekuwa mstari wa mbele kusema wamezuiwa kufanya mikutano ya hadhra".
Kwa upande mwingine, Polepole amewataka Wabunge waende kuishi kwenye majimbo yao ambayo wamepigiwa kura na wananchi wao ili waweze kuwasikiliza na kutatua kero zao ambazo wanakumbana nazo kwa madai hakuna njia nyingine mbadala wa hiyo huku akitolea mfano kwa kuwataja Wabunge wachache ambao hawaishi katika majimbo yao husika kuwa ni Zitto Kabwe, Freeman Mbowe, James Mbatia