CHADEMA Wadai Kushitushwa na Kauli ya "CCM Itatawala Milele"


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimesema kauli kuwa hadi ifikapo mwaka 2020 upinzani hautakuwepo na ile ya CCM itatawala milele, zinazidi kuwapatia mashaka. 


Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa CHADEMA , Benson Kigaila amesema kauli hizo na yale yanayojiri katika uchaguzi mdogo, vinawapa shaka kuwa kuna mpango usio wa heri.


“Tumepata nyaraka inayosambaa kwenye mitandao ina nembo ya Tume (ya Taifa ya Uchaguzi) na CCM wanaitumia kujitapa kushinda kata 30. Tunashindwa kuelewa kwa nini hatujapewa vyama inazunguka mitandaoni,”


Akizungumzia juu ya namna wanavyodhulumiwa  Kigaila amesema kwamba “Kata za Halmashauri ya Iringa Mjini pia wagombea wameondolewa kwa uonevu,”.


Hata hivyo kauli hii ya Bw. Kigaila inakuja ikiwa tangu siku moja ipite tangu Mwenyekiti wa UVCCM, Kheri Jame kusema kwamba CCM imejiandaa kupima ‘mitambo’ yake katika uchaguzi huo mdogo ili kuhakikisha inakifuta CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.


Katika kampeni hizo, James alisema kwamba “Nataka kuwaambia kwa namna mitambo yetu ilivyofungwa hakuna mgombea wa upinzani ambaye atashinda, na mwaka 2020 CHADEMA watabaki labda ya majimbo mawili tu kusini moja na kaskazini moja,”


Alisema katika kuhakikisha kazi zinafanyika vizuri, wabunge wa upinzani wataporomoka wote mwaka 2020 na CCM itakaa yenyewe ili kupitisha mambo ya maendeleo kwa Watanzania.


 Hata hivyo kauli Mwenyekiti wa UVCCM haijapishana na ya Mwenyekiti wa Chama hicho Rais John Magufuli  kwamba chama hicho kitatawala milele


“CCM ni chama tawala na kitaendelea kutawala milele na milele. Kwa wanaohangaika watapata tabu sana siku zote, siku hakuna mbadala ni CCM hadi milele. Wanachama wa CCM tembeeni kifua mbele tumeamua kuleta Tanzania mpya inayowapigania wananchi  hasa wanyonge ili waweze kushiriki katika maendeleo,”  alisema Dk. Magufuli.


Katika uchaguzi mdogo unaoendelea CHADEMA wamekuwa wakilalamika kuchezewa rafu na wapinzani wao huku wakieleza kwamba dola, pamoja na Tume ya uchaguzi imekuwa ikiwapendelea wenzao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad