Chin Bees Awapa Makavu Wasanii Wanaofanya Kiki Kutambulisha Kazi Zao

Chin Bees Awapa Makavu Wasanii Wanaofanya Kiki Kutambulisha Kazi Zao
MSANII wa Muziki wa Hip Hop Bongo, Musa Ramadhani ‘Chin Bees’ amechukizwa na baadhi ya wasanii wanaopenda kufanya kiki ili waweze kutambulisha kazi zao na kusema kuwa kufanya hivyo kunawapunguzia mashabiki.


Akizungumza na Over Ze Weekend, Chin alisema anashangaa kuona wasanii wenzake wakifanya kiki mitandaoni wakati muziki ni biashara ambayo inahitaji ubunifu tu ili uweze kufanya vizuri na mashabiki wafurahie muziki wako.



“Mimi nachukizwa kwa kweli, wasanii wapo kwenye biashara kwa hiyo ni bora ukafanya kazi kwa ubunifu kuliko kufikiri kiki ndio itakayokufanya ukauza nyimbo zako, unaweza ukatengeneza kiki na bado usifanye biashara ukawa umejishushia heshima tu,”alisema Chin.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad