Club ya Chelsea ya England leo Ijumaa ya July 13 2018 imetangaza rasmi kufanya maamuzi ya kuachana na aliyekuwa kocha wao mkuu Antonio Conte baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao kwa siku za usoni.
Antonio Conte anafutwa kazi Chelsea baada ya kudumu na club hiyo kwa miaka miwili na amefanikiwa kuiongoza Chelsea kutwaa taji la Ligi Kuu England msimu wa na Kombe la FA lakini Conte ameweka rekodi ya kuiongoza Chelsea kupata ushindi katika game 30 kati ya 38 za Ligi Kuu.
Taarifa zilizoripotiwa kuwa maamuzi hayo ya Chelsea kumfuta kazi Antonio Conte yatawagharimu Chelsea kumlipa Antonio Conte fidia ya pound milioni 9 ili kufidia sehemu ya mkataba wake uliyobaki.
Antonio Conte alijiunga na Chelsea mwaka 2016 baada ya kuacha kazi ya kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Italia, hivyo nafasi ya Conte inatajwa kuwa itarithiwa na Maurizio Sarri ambaye alikuwa kocha wa Napoli.