“Congo ingepata Rais kama Magufuli sijui ingekuwaje” –Christian Bella

Staa wa miondoko ya Dance Tanzania mwenye asili ya Congo Christian Bella amezimiliki dakika tatu za mahojiano na ripota wa Ayo TV na millardayo.com ambapo amezungumzia mtazamo wake kuhusu utendaji kazi wa Rais Magufuli pamoja na maamuzi ya Serikali kufungia nyimbo za wasanii.

“Rais Magufuli ni kama baba yangu, ukiachana na mambo ya kiserikali mimi nikiwa Congo sijawahi pata nafasi hata ya kuitwa na Rais lakini Rais Magufuli yeye ameweza kuniita na kupongeza kazi zangu yani hii ni kumbukumbu kubwa “-Christian Bella

“Kuna vitu vingi na vikubwa sana Rais Magufuli anavifanya ambayo ni mifano ya kuigwa ambapo sisi kama Congo tungempata mtu kama yeye ingekuwa vizuri sana.”-Christian Bella

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad