CUF Yatangaza Mgomo Zanzibar

Chama cha Wananchi (CUF) , kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa jimbo la Jang'ombe ambao unatarajiwa kufanyika Octoba 27 mwaka huu huku baadhi ya vyama vimesema vitashiriki vikiwemo vya CCM, Ada, TADEA, ADC, na AFP.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Salum Abdallah Bimani amesema kuwa chama hicho hakitoshiriki uchaguzi huo kutokana na kutoridhishwa na kitendo cha Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar  (ZEC), kufuta matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25 mwaka 2015.

 “Kufuatia uamuzi huo wa ZEC, Chama cha Wananchi, hakina imani na uchaguzi wowote wa Uwakilishi au Udiwani utakaofanyika Visiwani Zanzibar na wafuasi wa chama chetu hasa wale wa jimbo la Jang'ombe hawatoshiriki katika uchaguzi huo”, amesema Bimani.

Aliyekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Jangombe kupitia Chama cha Mapinduzi, Abdallah Diwani alifukuzwa uanachama Mei 29 mwaka huu na kupoteza nafasi ya Uwakilishi katika jimbo hilo na ndipo Tume ya Uchaguzi kuamuru kufanyika uchaguzi mdogo ili kuziba nafasi hiyo.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad