Diamond Azuiwa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Nchini Tanzania kwa Kukosa Kibali cha BASATA

Mwanamuziki nyota nchini Tanzania, Diamond Platnumz na msafara wake walikuwa katika hali ya taharuki kwa saa kadhaa baada ya kuzuiwa na Baraza la sanaa nchini Tanzania, BASATA walipokuwa kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwenda kutumbuiza nje ya nchi kwa kuwa hakuwa na idhini (kibali ) cha Baraza hilo.

Akizungumza na Shirika la Habari nchini Tanzania, TBC ,kaimu katibu mtendaji wa BASATA, Onesmo Mabuye, alisema ''msanii au kikundi chochote kinachotoka nje ya nchi kwa ajili ya maonyesho lazima kipate kibali cha BASATA ili ikaonyeshe kazi kule inakokwenda katika weledi ambao sisi tunaufahamu na tunafahamu habari ya ratiba ile ya kwenda nje ya nchi , si hivyo tu akimaliza shughuli zake kula nje anaporudi nchini anapaswa kurudisha taarifa BASATA''.

BASATA inasema kuwa msanii huyu 'hakuona kama jambo hilo ni muhimu' pamoja na kushughulikia safari yake alisahau kipengele hicho ambacho kina umuhimu wake.




Gazeti la mwananchi nchini Tanzania lilimnukuu Meneja wa mwanamuziki huyo, Babu Tale akisema Diamond alitakiwa kuondoka Alhimisi mwendo wa saa 3.00 asubuhi lakini baada ya kuzuiliwa ilibidi aondoke saa 11.00 jioni baada ya kukamilisha taratibu za kupata kibali hicho.

"Ni kweli jana msanii wangu (Diamond) alikumbana na mkono wa Basata akiwa uwanja wa ndege. Kwa kuwa tulishalipwa hela ya watu ikabidi tukishughulikie kibali haraka ili aweze kuondoka nchini,"alisema.

Hata hivyo, alilaumu Basata kwa kushindwa kuweka wazi kanuni zake ili wasanii wazijue badala ya kuwasubiri wakosee ili wawachukulie hatua.

Baadhi ya kanuni mpya za BASATA mwaka 2018

Vyombo vya habari havitaruhusiwa kupokea wala kurusha kazi za sanaa ambazo hazitakuwa na ithibati ya maadili kutoka Baraza
Baraza litatoa ithibati ya maadili ya sanaa kwa maandishi na kupigwa muhuri wa Baraza kwa kazi za sanaa zilizothibitishwa
Hakuna kazi ya sanaa itakayopelekwa sokoni ama kwa walaji bila kupewa kibali cha kuthibitisha kuwa maudhui yamezingatia maadili

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Basata vipi? Imani ya chama cha TANU inasema "kila mtu ana haki yay uhuru wa kwenda kokote ili mradi havunji sheria. Mngeweka vizuizi km hivyo kwa waingiao nchini, hiyo sijui

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad