Diamond Kuwakutanisha Wema na Zari Nchini South Africa
0
July 26, 2018
Ikiwa siku zinakaribia kuelekea birthday party ya mtoto wa staa wa Bongo fleva Diamond Platnumz na Bosslady Zarinah Hassan, Diamond anatarajiwa kuwakutanisha Zari na Wema nchini Afrika ya Kusini.
Diamond Kupitia uongozi wa label yake ya WCB imetangaza kusafiri na Wema Sepetu ambaye ametajwa kuwa mmoja wa wanakamati wa birthday party ya Tiffah Dangote.
WCB wamesema wataisafirisha kamati hiyo kwa kuwa wameipenda na wanaona ni jambo zuri kwenda kushiriki nao kwenye shughuli hiyo. Mastaa wengine ambao wanaunda kamati hiyo ni Shamsa Ford, Shilole, Irene Paul, Irene Uwoya, Lamata, Kajala Masanja pamoja na wengine wengi.
Wema pamoja na wanakamati wengine ambao siku ya jana walikuwa wanakamati katika arobaini ya mtoto wa Zamaradi wamepokea mualiko huo uliowasilishwa na Meneja wa Diamond Babu Tale.
Diamond ameitaja Birthday party ya Tiffah kama sherehe ya mwaka ambapo pia amehaidi kuwalipia mashabiki kadhaa kwa ajili ya kwenda kuhudhuria.
Tags