Kufuatia kuwepo kwa Vilio vingi vya wasanii wa Bongo Fleva Video zao kuondolewa kwenye mtandao wa Youtube, imeelezwa kuwa tatizo kubwa linalowasumbua ni kukosa elimu juu ya Ulimwengu wa Kidigitali.
Kushoto ni msanii, Q Chife, (Katikati ) ni Mtaalamu wa mambo ya mtandao Mx Carter na wa mwisho ni rapa Bilnass
Akizungumzia tatizo hilo katika mahojiano maalum na www.eat.tv mtaalamu wa masuala ya mtandao hasa Youtube Michael Mlingwa maarufu Mx Carter amefunguka kuwa kabla ya wasanii kulalamika wanatakiwa kujifunza vitu vingi hasa katika ulimwengu huu wa utandawazi ambao bado watu wengi hawajaufahamu vizuri matumizi ya mtandao huo.
Kauli hiyo ya Mx Carter inakuja wakati kuna baadhi ya wasanii wanaowalalamikia wasanii wenzao na wadau wengine kwamba wanawafanyia hujuma ambazo zinasababisha video zao kuondolewa youtube, pasipo kujua hayo ni mambo ya kitaalam ambayo hufanywa na youtube wenyewe baada ya kutokea matatizo mbalimbali.
Akitaja baadhi ya sababu zinazofanya Video kuondolewa Youtube Mx Carter amesema "kuna vigezo vingi hapa kwanza kabisa aina ya Video unayoweka (kama imezingatia maadili), pili wanaangalia ile video kama unamamlaka nayo sasa unakuta baadhi ya video umeweka wewe ndio mwenye video lakini unakuta watu wengi wamepakia youtube"
Amesema baada ya Youtube kuangalia video husika na kukuta inamakosa kulingana na sheria zao wanaweza kuindoa, lakini pia wanauwezo wa kuirudisha endapo mwenye umiliki halali wa video atajieleza vizuri.
Mx Carter ameongeza kuwa " Nafikiri sasa hivi watu wanalalamika sana kuhusu Viewer's ( watazamaji) kutokuongezeka hilo pia ni tatizo ambalo lipo kwa upande wa Youtube wenyewe wanaangalia labda umeweka Video yako ikaanza kuangaliwa kwa wingi, siku hizi wamebadilisha mfumo unaoangalia kile kifaa kinachotumika kuangalia video, Mfano wanajua kabisa mtu mmoja hawezi kutumia simu au Komputa kuangalia video moja mara 20 kwa muda huo huo"
Mx Carter amefafanua kuwa Youtube wakikutana na tatizo kama hilo wanachokifanya ni kupunguza kama uliangalia mara 20 wanapunguza zile 17 zinabaki 3 ndio maana muda mwingine Viewer's (watazamaji) wanasimama ili kupisha ule mfumo ufanye mahesabu yake hiyo video imeangaliwaje baada ya hapo wanaiachia kama kuna watazamaji walioangalia waukweli wanaendelea kuwepo.
Hata hivyo Wasanii ambao Nyimbo zao zimewahi kuondolewa kwenye mtandao wa Youtube katika siku za hivi karibuni ni pamoja na Billnass, Aslay na Q-chief
Elimu inavyowatesa Wasanii wa Tanzania, Malalamiko ya Youtube ni Elimu Ndogo
0
July 29, 2018
Tags