Akizungumza na Risasi Jumamosi, Faiza alisema hana njia nyingine ya kumfikishia ujumbe mzazi mwenziye huyo zaidi ya kwenye mtandao wa Instagram kwani ndio sehemu pekee ambayo atasoma na kumuelewa kwa umakini na huwa anafanya hivyo kwa sababu hakuna anayeweza kumfikishia ujumbe mzazi mwenzie huyo kwa kuwa wanamuogopa.
“Mimi sinaga namba yake na ndio maana huwa naandika Instagram sababu nahisi ndio sehemu sahihi kwani nikiwatuma watu wakamfikishie ujumbe huwa wanamuogopa nikaeleza kwamba aache kutumia watu mahitaji ya mtoto, alete mwenyewe mtoto amuone,” alisema Faiz