Faiza Ally Adai Sugu Atakuwa Amelogwa Vibaya Sana


Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Faiza Ally amerudi tena kwenye headlines na sakata la mzazi mwenzake ambaye ni Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu.

Faiza amemtolea povu zito Sugu na kudai atakuwa amelogwa maana matendo anayefanya sio ya kawaida hata kidogo na anaamini hakuwa hivyo zamani wakati wako wote.

Faiza amefunguka hayo baada ya sakata lao la juzi ambapo Faiza alimtolea povu Sugu Kwenye mitandao ya kijamii na kumtaka amuheshimu baada ya Sugu kumtuma Mke wake kufanya shopping ya Faiza badala ya kumpa pesa.

Kwenye mahojiano aliyofanya na kipindi cha Refresh cha Wasafi Tv, Faiza ameongea haya:

Kwa jinsi ninavyomjua Baba Sasha ni mtu ambaye ana akili zake lakini sijui labda kalogwa kwa sababu nilijua naye mpaka mtoto akakua kuwa na alikuwa responsible father kwa wakati huo kwa nini sasa hivi amekuwa na mwanamke mwingine amebadilika”.

Faiza aliendelea kuelekeza tuhuma za kulogwa kwa Sugu:

Mimi nadhani atakuwa amelogwa tena atakuwa amelogwa milogo mibaya ambayo yeye mwenyewe hajui kwa sababu katika hali ya kawaida huwezi kuleta matatizo Kwenye kumlea mtoto mwenyewe mmoja halafu uwezo unao kama hajalogwa atakuwa na matatizo ya akili”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad