Sugu na Faiza wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Sasha lakini wamekuwa kwenye mgogoro wa kifamilia kwa muda mrefu sana ambapo Faiza amekuwa akidai kuwa Sugu anagoma kumlea mtoto.
Wawili hao walionekana kumaliza tofauti zao mwezi uliopita baada ya Sugu kutoka jela ambapo Faiza aliandika Kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na Sugu wamemaliza tofauti zao.
Lakini Faiza amemtolea povu Tena Sugu jana ambapo kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika:
“Natuma barua kwako kwa sababu sehemu pekee ya kukufikishia ujumbe ukaupata ni hapa ni hivi toka tumeachana sasha ana mwaka na miezi 6 mpaka leo hujatafuta namna sahihi ya kumtunza mwanao sasa tafuta njia sahihi na yenye heshima mimi sio wa kufanyia shopping na happy eti nikachukue mlimani ”
“Hiyo ni zarau sana baba kama ulikosa muda ungetuma hela ! Lazima uweke heshima kwa baby mama wako na mwanao! sasa ni hivi siwezi kwenda kuchukua sukari na maziwa mlimani ni DHARAU!!!!!!”