Faiza Ataja Sababu Ya Kuanika Ugomvi Wake na Sugu Mitandaoni


Muigizaji wa Bongo movie na mjasiriamali maarufu Kwenye mitandao ya kijamii Faiza Ally amedai sababu inayompelekea yeye kuanika ugomvi wake ni Sugu mitandaoni ni kukosa njia nyingine ya kuwasiliana naye.

Faiza na Sugu wamezaa mtoto mmoja anayeitwa Sasha na kwa muda mrefu wawili ho wamekuwa Kwenye migogoro na migogoro yao huwa Ikiwa Kwenye mitandao ya kijamii.

Kwenye mahojiano na gazeti la Risasi Jumamosi, Faiza amedai hana njia nyingine ya kumfikishia ujumbe mzazi mwenziye huyo zaidi ya kwenye mtandao wa Instagram kwani ndio sehemu pekee ambayo atasoma na kumuelewa kwa umakini na huwa anafanya hivyo kwa sababu hakuna anayeweza kumfikishia ujumbe mzazi mwenzie huyo kwa kuwa wanamuogopa.

Mimi sinaga namba yake na ndio maana huwa naandika Instagram sababu nahisi ndio sehemu sahihi kwani nikiwatuma watu wakamfikishie ujumbe huwa wanamuogopa nikaeleza kwamba aache kutumia watu mahitaji ya mtoto, alete mwenyewe mtoto amuone”.

Siku chache zilizopita Faiza amemuanika Sugu Mtandaoni na kudai amelogwa baada ya kukataa kumpa fedha za matumizi ya mtoto wao.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Low class bitch, tujifunze wanaume kupitia huu mwanamke, siyo kila mwanamke ni wa kuzaa naye.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad