Familia ya Muna Waungana na Peter Zacharia Mwananyamala Katika Msiba wa Mtoto wao Patrick

Ndugu wa Muna Waungana na Peter Zacharia Mwananyamala  Katika Msiba wa Mtoto wao Patrick
Kufuatia kifo cha mtoto wa Muna Love, Patrick aliyeaga dunia juzi Nairobi,Kenya akipatiwa matibabu, taarifa zenye mkanganyiko zimekuwa zikisambaa mitandaoni kuhusu nani ni baba halisi wa mtoto huyo huku wengine wakisema ni Casto na wengine wakidai ni Peter Zacharia.

MCL Digital ilifunga safari mpaka Mwananyamala nyumbani kwa Peter Zacharia Komu, anayedai kuwa ni mume wa ndoa wa Muna na ndiye baba mzazi wa marehemu Patrick, huku akieleza amekuwa akimhudumia mtoto huyo kuanzia matibabu yote, matunzo na ada ya shule.

Alidai kuwa yeye ndiye baba wa mtoto kwa kuwa vielelezo vya kumuhudumia mtoto anavyo huku akisema, alimkatia Bima ya Afya ya Jubilee.

Peter ameiambia MCL Digital kuwa yeye ni mume halali wa Muna walifunga ndoa kanisani mwaka 2010.


Alisema Patrick alipozaliwa miaka saba iliyopita, hakutaka kujitokeza hadharani kubishana na Casto ila aliwahi kumwambia asiingilie familia yake,na kumwambia Muna kuwa akakanushe anachoandika Casto kuwa Patrick ni mwanae.

Lakini tangu Kifo kitokee kumetokea na utata mkubwa katika msiba wa mtoto huyo kwani misiba imewekwa sehemu mbili kwa Peter ambaye anadai Patrick ni mtoto wake na kwa Muna anadai mtoto wa Casto.

Kutokana na hayo, Ndugu wa Muna ambao ni mama mzazi,dada yake,kaka yake,wajomba na mdogo wake wameungana na Peter na kudai wao wanachofahamu baba halali wa Patrick ni Peter, Casto wanamsikia mitandaoni tena baada ya Patrick kufikisha miaka mitano.

MCL Digital ilipata kuongea na mama yake Muna,ambaye hakuwa na hali nzuri kwani kila wakati alikuwa anazimia na kuishiwa nguvu.

 “Huyu Peter ndiyo baba halali wa Patrick navyojua mimi, ila sifahamu Muna amepatwa na nini, kwani kitu anachokifanya siyo sahihi kwa Peter,wakati ukweli anaujua kabisa. Sielewi,sielewi kabisa Muna kwanini yuko hivi,” alisema.

MCL Digital haikuishia hapo, ilizungumza na dada wa Muna naye amefunguka na kubainisha kuwa familia inafahamu mtoto huyo ni wa Peter na siyo Casto.

Chanzo: Mwananchi

Top Post Ad

Below Post Ad