Feza Kessy Adai Kuumizwa na Skendo Za Kuwa Msagaji


Msanii wa muziki wa Bongo fleva Feza Kessy amefunguka na kudai anashangazwa na kuumizwa na skendo ambayo inamuandama Kwenye mitandao ya kijamii kuwa ni msagaji.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na tetesi kuwa Feza amekuwa Kwenye Mahusiano ya jinsia moja (Usagaji) na hata kuhusishwa kuwa Kwenye Mahusiano na msanii mwenzake Vanessa Mdee.

Kwenye mahojiano na kipindi cha Enews cha EATV, Feza amekana tena skendo hizo na kudai haelewi kwa nini watu wanamsingizia kuwa na tabia za ajabu kiasi hicho ilhali hajawahi kukubali kuwa msagaji.

Sio mara ya kwanza kusikia hizi taarifa hii ni kama mara ya pili au ya tatu lakini naomba nikanushe tena kiufupi sio kweli na sihitaji kujitetea sana.

Feza alipoulizwa sababu Gani watu wamekuwa wakimsingizia yeye tu anajihusisha na usagaji alifunguka:

Mara ya kwanza nilivyosikia watu wananisema hivyo ilibidi niulize kwa Nini labda au ni jinsi ninavyovaa au jinsi ninavyojiweka au ni watu ambao ninaojihusisha nao lakini sikupata jibu sahihi labda hao wananisingizia waniambie kwa nini labda”.

Lakini pia Feza amekana taarifa za yeye kuwa na uhusiano na Vanessa na kusisitiza yule ni rafiki yake wa siku  nyingi na zaidi ni kama dada yake ambaye anaheshimiana naye siku nyingi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad