Gabo Amefanikiwa Kuziba Pengo La Kanumba- Mama Kanumba

Gabo Amefanikiwa Kuziba Pengo La Kanumba- Mama Kanumba
Mama mzazi wa aliyekuwa staa wa Bongo movie Steven Kanumba, Flora Mtegoa maarufu kama Mama Kanumba amemtaja msanii ambaye anaamini ameziba pengo la Kanumba Kwenye tasnia ya Bongo movie.

Mama Kanumba ambaye naye aliingia Kwenye Bongo Movie mara baada ya mwanaye kufa amemtaja Gabo Zigamba kama Msanii ambaye ameziba pengo la Kanumba.

Kwenye mahojiano  na Wasafi TV, Mama Kanumba amemtaja Muigizaji wa Kiume Gabo Zigamba kama ndiye msanii pekee mwenye uwezo sawa na Kanumba kwa sasa.

Gabo anajitahidi kwa kweli, nilichogundua kwanza anajua kuuvaa uhusika kwenye filamu zake, akiwa kama mlinzi anakuwa mlinzi kweli, akiwa kichaa anakuwa kichaa kweli. Namwambia asikate tamaa kuna watu watamkatisha tamaa kila atapokaribia kuyafikia mafanikio zaidi.”

Lakini pia Mama Kanumba amelinganisha uwezo wa Kanumba na Gabo:

Ni kweli Gabo ‘anashika kijiti cha Kanumba’ anajitahidi, anauthubutu, anajaribu, anajituma na anaweza”.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad