Gabo atwaa Tuzo nyingine


Muigizaji nguli wa filamu Tanzania Gabo Zigamba ametunukiwa tuzo ya ushindi katika kipengele cha muigizaji bora wa kiume kupitia filamu aliyoigiza ya ‘SUMU’ kwenye tamasha la ZIFF lililofanyika visiwani Zanzibar.

Akizungumza na www.eatv.tv, Gabo ameweka wazi juu ya hatua zinazofanyika mpaka yeye kushinda tuzo hiyo licha ya filamu kuwa haijaangaliwa na watazamaji wengi na kusema hilo ni jambo la kawaida kufanyika kwa majaji duniani kote kupitisha filamu ambayo haijatazamwa na mashabiki.

"Tuzo zilivyo duniani zipo za aina mbili, zile za ‘Choice Awards’ kwa maana ya tuzo zinazopatikana kwa Kura za mashabiki kwa filamu walizoziona, na kuna tuzo zinazotolewa kwa kufanyiwa ‘judgement’ na watengenezaji filamu ambazo huchujwa hata kabla watazamaji hawajaziona kwa mara ya kwanza kwenye ‘Movie Premiers’. Mfumo huo hutumika duniani kote na ndio tuzo yenye hela sana na kubwa duniani ukiachana na tuzo zinazopatikana kwa kura za mashabiki, sababu kura wanazopiga mashabiki ni kipimo cha kujua watu wanakupenda kias gani", amesema Gabo.

Hii ni tuzo ya pili kwa muigizaji Gabo kutunukiwa katika rekodi za utolewaji wa tuzo za ZIFF ikiwemo tuzo ya muigizaji bora wa kiume kupitia filamu ya ‘SAFARI YA GWALU’ aliyoshinda mwaka 2016.

Hata hivyo mshindi mwingine katika tamasha hilo kutoka Tanzania ni muigizaji Catherine Credo mwenye umri wa miaka 21, ambaye amefanikiwa kutwaa tuzo ya muigizaji bora wa kike kupitia filamu ya Fatuma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad