Gari la Serkali Lililokamatwa na Mirungi LAMTUMBUA Mganga Mkuu Hospitali ya Mji wa Tarime na Wenzake Wawili


Mkurugenzi wa Halamshauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa

**

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa amewasimamisha kazi watumishi watatu akiwimo kaimu mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime baada ya gari la wagonjwa la Hospitali hiyo kukamatwa likisafirisha  dawa za kulevya aina ya mirungi Wilayani Bunda Mkoani Mara Julai 11 Mwaka huu.


Waliosimamishwa kazi ni Kaimu Mganga Mkuu (DM) Dkt Innocent Kweka, Kaimu Mganga Mfawidhi Dkt Amir Kombo na katibu wa Hospitali Rwegasira Karugwakutokana na uzembe waliofanya mpaka kitendo hicho kinafanyika.


“ Namsimamisha kazi DMO, Mganga Mfawidhi na Katibu wa hospitali kuanzia leo hadi tuakapomaliza uchunguzi wetu ambao umeanza kubaini kwa nini gari la wagojnwa lilitumika kusafirisha madawa ya kulevya .Kama hawana hatia watarudi kazini”alisema Mkurugenzi.


Ntiruhungwa amesema hawezi kuvumilia kitendo hicho ambacho kimechafua jina la Hamashauri yake na nchi kwa ujumla na kwamba yeyote ambaye atabainika kuhusika katika tukio hilo atachukuliwa hatua kali.


Ameongeza kuwa tayari suala hilo linafanyiwa uchunguzi wa kina ili kubaini dereva huyo George Matai alipataje fursa ya kusafirisha madawa ya kulevya kwa kutumia gari la wagonjwa na kusema kuwa tayari amemsimamisha kazi kuanzia leo.


Mkurugenzi huyo aliwataka wakuu wa idara katika Halmashauri yake kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuepuka vitendo vya aibu kama hivyo kutokea tena.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad