Hatimae Yanga imetoa List ya Wachezaji Wake 2018/19

Club ya Dar es Salaam Young Africans ikiwa siku moja imepita toka dirisha la usajili lifungwe, leo imetaja list ya wachezaji wake itakaowatumia msimu wa 2018/2019, huku ikimteua nahodha wao Nadir Haroub Canavaro kuwa meneja mpya wa timu yao.

Yanga imewasajili jumla ya wachezaji wapya saba huku ikiachana na wachezaji wake wanne ambao ni Hassani Kessy aliyemaliza mkataba wake na kwenda kujiunga na club ya Zambia, Obrey Chirwa aliyemaliza mkataba wake na kwenda Misri.

Wakati kwa upande wa Geofrey Mwashiuya amemaliza nae mkataba wake na kujiunga na Singida United huku Mzimbabwe Donald Ngoma wakivunja nae mkataba kutokana na kuwa majeruhi kwa muda mrefu, Ngoma kwa sasa amejiunga na Azam FC

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad