Hatimaye Boeing 787-8 Dreamliner Kutua Leo Tanzania

RAIS Dkt. John Magufuli leo Jumapili Julai 08, 2018 atawaongoza watanzania katika mapokezi ya ndege mpya aina ya Boeing 787-8 Dreamliner iliyonunuliwa na serikali ya Tanzania.

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa alasiri ya jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu ya Rais, Gerson Msigwa na kusema ndege hiyo inatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam majira ya saa 8:00 mchana leo ikiwa inatokeaa Seattle nchini Marekani.

Hii ni ndege ya nne kuwasili nchini kati ya ndege 7 zilizonunuliwa na serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuliwezesha Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kuimarisha huduma zake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad