Hatimaye Watoto 12 pamoja na Mwalimu Wao Waliokwama Pangoni Siku 18 Waokolewa Wote


THAILAND: Hatimaye Watoto 12 pamoja na Mwalimu wao wa mpira wa miguu walikuwa wamekwama kwenye pango lililokumbwa na mafuriko wameokolewa.

Watoto hao waliokwama mnamo Juni 23 walianza kuokolewa kwa makundi na hatimaye mchana huu kundi la mwisho limefanikiwa kutoka ndani ya pango hilo.

Watoto 8 waliokolewa siku ya Jumapili na Jumatatu huku wakiwa na afya njema ya akili na mwili

Wanajeshi wa Kikosi cha Maji walifanikiwa kuwapelekea chakula mara baada ya kutambua umbali walopo kabla ya juhudi za uokozi kuanza

Watoto hao walikwama umbali wa Kilomita 4 kutoka kwenye mdomo wa mpango hilo

Siku ya Ijumaa Mwanajeshi mmoja wa kikosi cha uokoaji alifariki dunia kwa kuishiwa na hewa ya Oksijeni wakati akiwa kwenye harakati za zoezi la uokoaji

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad