Hawa Ndio Vinara wa Masomo ya Sayansi Kidato cha Sita

Hawa Ndio Vinara wa Masomo ya Sayansi Kidato cha Sita
Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) limetangaza matokeo  ya kidato cha sita leo Julai 13 na kutoa orodha ya watahiniwa waliofanya vizuri zaidi kitaifa katika mtihani huo.

 Katibu Mtendaji wa Necta, Charles Msonde, ametangaza matokeo hayo akiwa visiwani Zanzibar leo.

 Watahiniwa waliofanya vizuri  zaidi kitaifa katika masomo ya Sayansi ni pamoja na Anthony Mulukozi, wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Asia Jasho wa Tabora Girls, na Raphael Fanuel wa Ahmes, Pwani.

Wengine waliofanya vizuri ni pamoja na Godfrey Kawau, Uru Seminari, Kilimanjaro na Biubwa Hamis Ussi, wa shule ya Sekondari ya Sos Hermain Gmeiner, Mjini Magahribi (Zanzibar).

Wengine ni Fahad Rashid Salum, shule ya Sekondari Lumumba, Mjini Magharibi, Prince Walter Ngao, Marian Boys, Pwani, Victor Maghembe, Marian Boys, Pwani na Emmy Shemdangiwa, St Marys Mazinde Juu, Tanga na Vanessa Lodrick Shoo wa St Marys, Mazinde Juu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad