Haya Hapa Madhara Makubwa yanayowapata Wanaokula Mirungi


AFYA: Je, unayajua madhara ya kiafya anayoyapata mtumiaji wa Mirungi

Mirungi ni mmea ambao una majina mengi kulingana na eneo. Mfano; gomba, miraa nakadhalika

Ulaji wa mirungi unadaiwa kuanzia nchini Ethiopia, ukaenea hadi nchi za Afrika Mashariki, Yemen, Zimbabwe, Zambia, Malawi na hata Afrika kusini

Mirungi ilionekana kuwa ni moja ya madawa ya kulevya hivyo ikakatangazwa na umoja wa mataifa UN na kupigwa marufuku mwaka 1971 kwasababu ya ufanano wa kemikali iitwayo amphetamine

Yafuatayo ni madhara ya kiafya ya mirungi kama ilivyofanywa na shirika la afya duniani kama ifuatavyo;

1. Mtumiaji wa mirungi yupo katika hatari ya kupata vidonda vya tumbo
-l
2. Kupungukiwa msukumo wa kufanya tendo la ndoa(low sex drive) na pia kuwahi kumaliza haraka na kutoweza kudumu kwenye tendo la ndoa kwa muda mrefu

3. Ukosefu wa haja kubwa(constipation)

4. Utumiaji wa muda mrefu husababisha ini kushindwa kufanya kazi na pia meno kubadilika rangi, kudhoofika, fizi kuuma na harufu mbaya mdomoni

5. Upungufu wa usingizi

6. Madhara ambayo bado kinamama walaji Mirungi hawajagundua ni kwamba mtoto anayezaliwa na mama mlaji Mirungi mara nyingi hukataa kunyonya titi la mama yake kwa sababu ladha ya maziwa inabadilika kwa ajili ya utumiaji wa madawa(pesticides) unaotumiwa na wakulima wa Mirungi kama inavyoeleza utafiti uliofanyika na Chuo Kikuu Cha Aden(Aden University)

Aidha,Utafiti mwengine kule Ethiopia unaeleza kuwa mtoto wa mama mwenye kula Mirungi kwa wingi huwa hana uzito wa kawaida wakati wa kuzaliwa

7. Ukosefu wa hamu ya kula chakula

Hayo ndio madhara yanayoelezwa kutokana na utumiaji wa mirungi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad