Hii ndio kauli ya Ndugai baada ya Waitara kujiuzulu


Ikiwa zimepita siku mbili tokea kujiuzulu kwa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limesema limepokea barua rasmi leo ya Waitara. 

Hayo yamebainishwa na taarifa zilizotolewa na mtandao wa kijamii wa Bunge ukisema kwamba Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amepokea barua hiyo na kuahidi kumuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kusudi aweze kuendelea na taratibu zingine. 

"Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amesema kuwa leo asubuhi amepokea barua ya kujiuzulu Ubunge wa Jimbo la Ukonga kutoka kwa Mhe. Mwita Waitara na hivyo atamwandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ili aweze kuendelea na taratibu zingine", imesema taarifa hiyo. 

Waitara anakuwa Mbunge wa pili CHADEMA, kujivua ubunge ambapo Mbunge wa kwanza alikuwa Dk. Godwin Oloyce Mollel ambaye Disemba 14, 2017 alitangaza kujivua rasmi uanachama wa Chama hicho na kujiunga na CCM kwa madai ya kuunga mkono utendaji ya Rais Magufuli. 

Kwa kipindi cha takribani miaka mitatu tayari wabunge wanne wameshajivua nyadhifa zao, ambapo dimba lilifunguliwa na Lazaro Nyalandu kutoka CCM kwenda CHADEMA, Maulid Mtulia CUF kuelekea CCM, Godwin Mollel CHADEMA kwenda CCM na sasa Waitara kutoka CHADEMA kuhamia CCM.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad