Hizi Hapa Kero Kubwa Katika Saloon za Kiume

Kama kichwa cha habari kinavojieleza...kwakweli kuna tabia za vinyozi hua zina kera sana unapokua umeenda kupunguza nywele...

1; Unakuta kinyozi .anapokea simu anaanza kuongea huku anaendelea na kazi ya kukata nywele au anaweza akastop kazi husika na akaendelea kuongea na simu,na unakuta maongezi ya kipuuzi tu...kwakweli inakera sana!

2; Vinyozi wavivu,yeye kazi yake ni kukuzungusha kichwa kama steering vile anaendesha gari...yani yeye hataki kuzunguka,au hata kuzungusha kiti...kazi yake inakua ni kukuzungusha kichwa utasema anataka kuking'oa...kwakweli inakera.

3; Mashine mbovu mbovu, imekua tatzo sana ktk saloon nyingi skuiz...unakuta mashine inabadili mlio afu kinyozi anastop anachukua screw driver anaanza kuikaza kaza baadhinya nati...ikikaa sawa anaendelea na zoezi hilo ni endelevu...inaboa sana!

4; Kinyozi unakuta anakupitishia waya wa mshine mara shingoni,mara unapita kifuani,mara aushike aurishie kati kati ya miguu yako...inakua kero ...hajui kua ule ni umeme cjui...


Kwakweli kero ni nyingi wadau...leteni zenu hapa nahisi wahusika wakisoma watajirekehisha!

By The_forum

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad