Hizi Hapa Sababu za Madiwani Watatu Kuvuliwa Uanachama CUF

Hizi Hapa Sababu za Madiwani Watatu Kuvuliwa Uanachama
Chama cha Wananchi (CUF) kimewavua uanachama wa chama hicho Madiwani watatu mkoani Tanga kwa kosa la utovu wa nidhamu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi Kuu za chama hicho kwa niaba ya vijana wa Jumuiya za Wilaya za DSM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Ilala (JUVICUF), Canal Kitimai amesema Madiwani hao ni Rashid Hamza wa Kata ya Mwanzange na Madiwani wawili wa viti maalum wa Wilaya ya Tanga ambao ni Halima Mbwana na Fatuma Hamza.

“Kutokana na Katiba ya CUF ya mwaka 1992 toleo la mwaka 2014 ibara ya 83 kifungu cha (4) nanukuu ‘Baraza Kuu l uongozi la taifa linaweza kuchukua hatua za kinidhamu zilizo zilizoainishwa katika kifungu cha (5) cha kifungu hiki dhidi ya viongozi watokanao na CUF.” -Kitimai

Hatua zinazoweza kuchukuliwa na Baraza la Uongozi la Taifa la CUF zilizoainishwa katika kifungu cha (5) dhidi ya kiongozi yoyote aliyetajwa kwenye kifungu cha (4) ni pamoja na kutoa onyo kwa maandishi, kutoa karipio kali kwa maandishi, kumsimamisha au kumfukuza uanachama.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad