Hizi ndio Sababu za Wanafunzi kufeli


OFISA elimu wa Mkoa wa Shinyanga, Mohamed Kahundi, amesema uongezeko la sifuri katika shule za serikali husababishwa na usimamizi mbovu wa walimu wakuu katika vituo vyao vya kazi sambamba na kujihusisha na vitendo vya kufanya mapenzi baina yao na wanafunzi. 

Tusiposimamia ipasavyo elimu kwa kufuata misingi yake, shule za serikali zitaendelea kupata ziro kila mwaka hata kama tutakuwa na malengo mazuri, na kwamba shule za watu binafsi zitaendelea kutubeba kutokana na kuwa na usimamizi mzuri wa walimu wakuu na kuwahimiza walimu wao kufundisha. 

Kahundi aliyabainisha hayo juzi katika kongamano la kuongeza ufaulu wa jimbo la Ushetu na kutokomeza sifuri katika shule za sekondari, lilijumuisha walimu wakuu wa shule, maofisa elimu kata, walimu wa taaluma, wenyeviti wa kamati za shule pamoja na Mbunge wa jimbu hilo ambae pia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa. 

Alisema walimu wakuu wengi wamekuwa wakishindana kuvaa suti na kuzurura katika halmashauri badala ya kuwasimamia walimu wao kufundisha na wakati mwingine wamekuwa wakiwagawa walimu, hali ambayo imekuwa ikitengeneza matabaka baina ya walimu na walimu badala ya kufundisha. 

“Kushuka kwa ufaulu wa elimu katika shule zetu za serikali unatokana na usimamizi mbovu wa walimu wakuu sambamba na kujihusisha na vitendo vya 

mapenzi baina yao na wanafunzi, na ikishafikia hatua hiyo wanafunzi hawezi kusoma na badala yake atakwenda kufanya vibaya katika mitihani yake ya mwisho,” alisema. 

Aliongeza: “Mheshimiwa waziri unakuta msimamizi wa kituo anakuwa na makundi ya walimu na hali hiyo ndio inapelekea wale wanaopendwa na mwalimu mkuu kushindwa kuhudhuria vipindi vyao darasani, sasa nawaagiza walimu kuvunja makundi na tunataka kuona ufaulu wa wanafunzi unaongezekana. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu, Michael Matomora, alisema asilimia kubwa ya wananchi wa Ushetu ni wafugaji ambao wamekuwa na maisha ya kuhamahama na hali hiyo imekuwa ikisababisha baadhi ya wanafunzi kukosa masomo kutokana na wazazi wao kuhama na kutafuta malisho ya mifugo yao. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad