Socialite maarufu kutoka pande za +254 Kenya, Huddah Monroe amewatolea uvivu wabongo kwa vitendo vya kinafki walivyomfanyia Jokate Mwegelo mara baada ya kuteuliwa kuwa mkuu wa wilaya.
Huddah amewatolea povu watu waliomnanga Jokate baada ya Ali Kiba kumuoa mwanamke mwingine ambaye ni Amina mwaka huu na kusababisha watu kumcheka sana Jokate.Kupitia Kwenye ukurasa wake wa Snapchat Huddah ameandika ujumbe huu:
“ Ali Kiba alivyomuoa msichana mwingine mapema mwaka huu watu walimcheka sana na kumdhalilisha Jokate. Lakini sasa hivi anapata mafanikio hao hao watu wanageuka na kumpongeza ama kweli mitandao imeshindikana. Hana mashabiki wa kweli bali ni wanafiki tu na wanaondoka kwa upepo”.
Ali Kiba alikuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na Jokate kwa muda mrefu lakini mapema mwaka huu alimuoa Amina.
Wikiendi iliyopita Rais Magufuli alimtangaza Jokate kama Mkuu wa wilaya ya Kisarawe jambo lilipelekea kupata pongezi nyingi sana kutoka kwa mashabiki mbali mbali na hata wasanii wenzake.
ndiyo wabongo walivyo walimsema sana Jokate wakati Ali kiba alioa mwanamke mwingine mpaka Jokate akakaa kimya na Mungu yupo kamjalia sasa amepata kazi nzuri na kazi aliyoipata Jokate ni kazi nzuri sana kuliko kuolewa na Ali kiba hata huyo Ali kiba mwenyewe na yeye angetamani kuwa mkuu wa wilaya lakini bahati hiyo kaipata mtu anayestahili ni Jokate mwegelo
ReplyDelete