Hukumu ya Kesi ya Wema Sepetu Kutolewa Leo

Hukumu ya Kesi ya Wema Sepetu Kutolewa Leo
Mahakama ya kisutu mjini Dar es Salaam inatarajiwa kutoa hukumu dhidi ya kesi ya umiliki wa bangi inayomkabili aliyekuwa mshindi wa shindano la malkia wa urembo nchini Tanzania Wema Sepetu.

Hakimu mkaazi Thomas Simba aliambia mahakama hiyo siku ya Jumatatu kwamba hukumu hiyo iliotarajiwa kutolewa siku ya Jumatatu sasa itatolewa Ijumaa baada ya kukamilika kwa maswala machache yaliokuwa yamesalia.

Wema Sepetu ambaye alishinda taji la malkia wa urembo nchini humo 2006 atahukumiwa pamoja na washtakiwa wengine wawili Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abas .

Inadaiwa kwamba mnamo tarehe 4 mwezi Februari mwaka uliopoita , Wema na wenzake walipatikana wakimiliki misokoto ya bangi katika eneo la Kunduchi Ununio.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad