Huyu Rais Mpya wa Mexico Kauzu Kweli, Akataa Ulinzi wa Aina yoyote, No Bodyguards na Usalama wa Taifa


Mexico City, Mexico. Rais mteule wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador ambaye ameahidi kukaribisha mageuzi nchini mwake amesema raia wa kawaida wa nchi hiyo ndiyo watakaomlinda na wala hapendelei kuona kikosi au kitengo chochote maalumu kikiandaliwa kwa ajili ya kuhakikisha ulinzi wake.

Rais huyo alipata ushindi wa kishindo katika uchaguzi uliofanyika Julai 1, amekuwa akitembea mitaani na kukutana na watu huku akiwa hana walinzi wowote. Katika safari zake hizo amekuwa akizunguka na gari yake aina ya Volkswagen Jetta na hakuna kizuizi chochote kinachoweza kukwamisha kukaribiwa na watu.

Katika tukio la karibuni, mmoja wa wafuasi wake alifanikiwa kuwapita walinzi waliokuwa katika jengo la Ikulu na kumkaribia na kisha kumkumbatia. Alikuwa amekwenda Ikulu kukutana na Rais anayemaliza muda wake, Enrique Pena Nieto.

Akizungumzia tukio hilo, Lopez Obrador alisema “Ngoja sauala hili liwe wazi. Sihitaji walinzi. Inamaanisha kuwa wananchi ndiyo watakaonilinda mimi,” alisema mwanasiasa huyo ambaye ataapishwa Disemba 1. Aliongeza akisema “Matumaini yangu hawatanidhuru,”. Kitendo chake hicho cha kukataa walinzi kimekosolewa vikali na baadhi ya wataalamu wa masuala ya usalama wa taifa na ulinzi wa viongozi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad