Idadi ya Vijana Waliookolewa Kutoka Pangoni Thailand Yafikia 10

Idadi ya Vijana Waliookolewa Kutoka Pangoni Thailand Yafikia 10
Vijana wengine wawili  waliokuwa wamenasa pangoni wameokolewa mchana huu na hivyo kufanya idadi ya waliookolewa kufikia kumi tangu kuanza kwa operesheni hiyo Jumapili iliyopita.

Vijana hao wanapatiwa matibabu ya dharura kabla ya kusafirishwa kwa helkopta kupelekwa hospitalini kuungana na wenzao wanaoendelea kuchunguzwa afya zao.

Wawili kati yao wamegundulika kuwa na matatizo kwenye mapafu na tayari wameanza kupata matibabu.

Kuokolewa kwa vijana hao kunafanya vijana waliokwama kwenye pango hilo kubakia wawili na mwalimu wao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad