Inasikitisha Ndugu Waifaa Polisi kwa Kifo cha Utata cha Ndugu Yao

Unaweza kufananisha na filamu ya kusisimua lakini hiyo haibadili ukweli, kwamba vijana watatu, Ismail Linyembe, Twahir Said na Idd Said hawapo tena duniani, wamefariki wakiwa mikononi mwa polisi katika tukio lililogubikwa na wingu zito la utata.



Julai 18, ni siku ambayo miili ya vijana hao, ilienda kuzikwa na kusababisha huzuni kubwa na simanzi kwa ndugu, jamaa, marafiki na wakazi wa Mbagala jijini Dar es Salaam, walikokuwa wakiishi vijana hao. Ni nini hasa kilichosababisha vifo vya vijana hawa watatu? Nini kilichowapata? Inaelezwa kwamba chanzo cha yote ni simu!


Simu ya mkononi imezaa mauaji, Ismail, Twahir na Idd, hawapo tena duniani lakini chanzo cha yote ni simu. Kwa mujibu wa mashuhuda, tukio hilo lilianza kama masihara hivi. Ilikuwa hivi, kijana mmoja aitwaye Kashi, alimpa simu Idd ambaye ni miongoni mwa vijana waliouawa, kwa makubaliano kwamba aende kuiza kisha amletee fedha zake.



Hata hivyo, inadaiwa kwamba marehemu hakutimiza makubaliano hayo, baadaye wawili hao walikutana ana kwa ana na ugomvi mkubwa ukazuka kati yao. Katika ugomvi huo, Kashi alimjeruhi kwa panga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad