Israel Yapitisha Sheria Yenye Utata Inayoliidhinisha Taifa Hilo Kuwa la Wayahudi Rasmi

Israel Yapitisha Sheria Yenye Utata Inayoliidhinisha Taifa Hilo Kuwa la Wayahudi Rasmi
Bunge la Israel limeidhinisha mswada unaokumbwa na utata wa kuiliidhinisha taifa hilo kuwa la kiyahudi.

Sheria hiyo mpya inaelezea bayana kwamba Israel ni taifa la wayahudi na inapunguza hadhi ya kiarabu kama lugha rasmi.

Sheria hiyo pia inatambua makazi ya wayahudi kwa maslahi ya kitaifa na kwamba Jerusalem ndio mji mkuu wa taifa hilo.

Wabunge wa Israel wenye asili ya kiarabu wamelaani vilkali sheria hiyo, lakini waziri mkuu waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameisifia sheria hiyo akisema ni "utambulisho wa aina yake".

Mswada huo, unaoungwa mkono na serikali ya mrengo wa kulia, unaeleza kuwa "Israel ni amkaazi ya kihistoria ya wayahudi na wana haki ya kiepekee ya kujitambua kitaifa wakiwa ndani ya nchi".

Ulipitishwa baada ya mjadala uliogubikwa na utata mkubwa katika bunge la Knesset uliodumu kwa zaidi ya saa nane. Wabunge 66 waliuunga mkono mswada huo huku 55 wakiupinga.

Hatahivyo baadhi ya vipengee vilitupiliwa mbali kufuatia pingamizi iliyozuka kutoka kwa rais wa Israel na mkuu wa sheria nchini, ikiwemo kipengee ambacho kingejumuishwa kwenye sheria cha kuundwa jamii za kipekee za wayahudi.

20% ya idadi jumla ya watu nchini humo inajumuisha waarabu wa Israel.

Mfanyakazi azawadiwa gari na mwajiri wake baada ya kutembea umbali wa kilomita 32

Kwa mujibu wa sheria hiyo wana haki sawa nchini, lakini kwa muda mrefu wamekuwa wakilalamika kuchukuliwa kama raia wasio kamili na wanasema wanakabiliwana unyanyasaji na huduma duni kama vile elimu, afya na makaazi.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad