Jaji Kiongozi, Dk. Eliezer Feleshi ambapo amewataka madalali na wasambaza nyaraka za mahakama kuacha kulalamika na kunung’unika badala yake wajenga hoja kuhusu changamoto zinazowakabili.
Dk. Feleshi ameyasema hayo wakati wa kuzindua mafunzo kwa madalali wa mahakama yaliyoandaliwa na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) katika kituo cha mafunzo na habari kilichopo Mahakamani Kisutu.
Dk. Feleshi amesema madalali wanatakiwa kuwa na uwezo kukamata mali za aina yoyote na sehemu yoyote hata kama itakuwa nje ya nchi.
“Ndio maana yameandaliwa haya mafunzo lengo likiwa kuwapatia umahiri katika utekelezaji wa majukumu yenu,” amesema.
Dk. Feleshi amewataka madalali kuendesha mijadala na kutumia fursa vizuri katika mafunzo badala ya kulalamika na kunung’unika.