Jeshi la Polisi Dar Lawatia Mbaroni Wahalifu Mbalimbali Wakiwemo 12 wa Mtandao wa Wizi wa Magari

Jeshi la polisi Kanda Maalum limewakamata watuhumiwa mbalimbali wa uhalifu wakiwamo 12 wa mtandao wa wizi wa magari na walioiba viatu vyenye thamani ya Sh 600 milioni.

Akizungumza na wanahabari jana Julai 11, Kaimu Kamanda wa polisi, kanda maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas alisema  Mei 23 polisi walikamata watuhumiwa hao wakiwa na katoni 500 za viatu zenye thamani ya Sh600 milioni zilizoibwa kwenye ghala la kampuni ya Bata Mei, 21.

“Watuhumiwa hao pia walikamatwa na gari aina ya mistubishi canter T 686 BWY ambalo lilikuwa limebeba mizigo hiyo pamoja na katoni 71 za bia mifuko 18 ya sabuni ya unga,injini 4 za pikipiki,na maboksi 61 ya nguo za mitumba”amesema

Kadhalika alisema Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa 12 wa mtandao wa wizi wa magari na pikipiki katika maeneo mbalimbali ndani na nje ya mkoa wa Dar es salaam.

Kamanda Sabas amesema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa upelelezi utakapokamilika watafikishwa Mahakama

Pia jeshi hilo la polisi limemkamata Omwalimu Binyakusha mmiliki wa Kampuni ya Arise Special Sunrise Safaris kwa kuwatapeli raia wawili wa kigeni.

“Mtuhumiwa huyu alichukua fedha kwa raia hao wa kigeni kwa makubaliano ya kuwapeleka safari lakini mwishoni aliwatelekeza hadi Serikali ilipoamua kuwahudumia,”amesema Sabas.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad