JEURI YA PESA: Diamond kutumia mil. 150 kwenye Birthday ya Tiffah, Harmonize akifanya ‘shopping’ ya mil. 100 Afrika Kusini
0
July 27, 2018
Kwa sasa ukizungumzia wasanii wenye fedha nchini Tanzania huwezi kuacha kuwataja Harmonize na Diamond Platnumz, na hili linaonekana wazi hata kwenye matumizi yao ya kawaida.
Siku za hivi karibuni Diamond Platnumz ametangaza kuwapeleka watu 50 kutoka Tanzania kwenda Afrika Kusini ambapo kati ya watu hao 30 ni mashabiki wake na 10 watakuwa ni wanakamati wa tukio ambao wataongozana na watoto wao.
Anyway! tupige mahesabu ya kawaida ya nauli ya mtu mmoja ya kwenda Afrika Kusini na kurudi kwa ndege. Kwa nauli ya chini ya daraja la Economy ni dola $600 sawa na tsh milioni 1.350.000.
Ambapo ukizidisha kwa watu 50 utapata milioni 67.5. Gharama za kuishi Afrika Kusini kwa siku tatu kwa watu 50 yaani kuanzia tarehe 17 hadi 19, 2018 kwa hoteli ya bei ya chini ni dola $150 kwa siku ambapo kila mtu kwa siku tatu atatumia dola $450 kwa ajili ya malazi, ambayo ni sawa na tsh 1.2 .
Ukipiga mahesabu ya kawaida ya kila mtu milioni 1.2 ya malazi kwa watu 50 unapata kama tsh milioni 60 na hapo bila gharama ya chakula. So roughly kuwagharamia watu 50, Diamond atatumia si chini ya milioni 150 kwa fedha ya kitanzania ili kukamilisha zoezi la kuwasafirisha watu 150 .
Wakati hayo yakijiri, msanii mwingine kutoka WCB, Harmonize yeye ameonekana akitumia fedha zake kwa matumizi mengine kabisa ikiwemo kununua nguo kutoka kwenye Clothing brand za gharama ya juu kabisa.
Harmonize unaweza ukasema ndio msanii kwa sasa Tanzania ambaye anafululiza kuvaa bidhaa za Gucci ambazo ni moja ya bidhaa za nguo zenye gharama kubwa duniani.
Tuanzie hapa! mwezi uliopita Harmonize alifanya shopping kwenye duka kubwa la bidhaa za Gucci nchini Afrika Kusini ambapo kwa kawaida hauwezi kuingia kwenye maduka hayo ya bidhaa za bei ghali duniani kama hauna dola $30,000 yaani zaidi ya tsh milioni 60.
Hii ndio maana hata baada ya kutoka kwenye duka hilo Harmonize mwenyewe alikiri kuwa bidhaa zao ni ghali sana ingawaje, ndio bidhaa azipendazo sana.
Tags