Jike Shupa'Waliotembea na Mimi Wapime Ukimwi'


VUTA picha ‘umetembea’ na mwanamke halafu ghafla anakwamba ukapime Ukimwi, utakuwa kwenye hali gani? Ndivyo alivyoibua mshtuko msanii wa filamu za Kibongo, Zena Abdallah ‘Jike Shupa’ baada ya kuibuka na kusema; “wanaume niliotembea nao kimapenzi zamani na sasa, wakapime Ukimwi ili kujua afya zao.”

NI WIKI ILIYOPITA

Kauli hiyo aliitoa msanii huyo mara baada ya kuachia picha yake ya nusu utupu katika mtandao wa Instagram inayoonyesha vipele na makovu maeneo ya mapaja, mwishoni mwa wiki iliyopita.



YAIBUA GUMZO

Dakika chache baada ya kuweka picha hiyo, gumzo la aina yake liliibuliwa na wafuasi wa mtandao huo huku kila mtu akieleza lake.

Kuna ambao walimchamba kwa kumwambia anajidhalilisha kwa kuweka picha za nusu utupu wakati anajua kabisa sheria zinakataza.

“Huyu naye vipi? Hata kama ndio kutafuta umaarufu sio kwa staili hii, anajitafutia tu matatizo maana siku hizi sheria zinawabana sana wasanii wanaoendekeza kujiachia utupu,” alichangia mdau mmoja mtandaoni.


WENGINE WACHOMEKEA YA UKIMWI

Kwenye wengi huwa hakukosi jambo, mbali na waliomtukana Jike Shupa na kusema amejidhalilisha, wapo wengine waliojiongeza kwa kutazama picha hiyo kwa jicho la tatu na kumhusisha msanii huyo na ugonjwa wa Ukimwi.

“Hebu angalia hivi vipele vilivyomtoka huyu atakuwa na ngoma tu si bure,” alichangia mdau mwingine mtandaoni huku akiungwa mkono na wafuasi wengine kibao.

Kuanzia hapo, upepo ukageuka kutoka kwenye ishu ya picha za utupu na moto wa Ukimwi ukawaka kama vile wa petroli.



VIGOGO, MASTAA MATUMBO JOTO

Kutokana na mjadala huo kuwa mkubwa mtandaoni, waliibuka wachangiaji mbalimbali walioeleza jinsi mastaa na vigogo mbalimbali ambao wanaaminika wamewahi kubanjuka na mrembo huyo jinsi walivyopata presha.

“Jamani nyinyi mnachangia lakini kuna mastaa na vigogo kibao ambao wamewahi kutembea naye humu sasa hivi matumbo joto, kama yule (anamtaja jina) na yule (anataja jina la msanii mkubwa) hali ni mbaya sasa hivi nyie mnashabikia tu humu,” alichangia mchangiaji mmoja mtandaoni.



HUYU HAPA JIKE SHUPA

Mjadala huo umelifanya gazeti hili limtafute msanii huyo ili kujua siri ya kuweka picha hiyo iliyozua mjadala mtandaoni na alipopatikana live, akafunguka kama ifuatavyo:

Ijumaa Wikienda: Habari za siku Jike Shupa, kuna hii picha yako iko mtandaoni, unaonekana uko nusu utupu mapaja yalionekana yana vipele vingi na makovu. Picha hiyo imezua mjadala sana. Kwa nini uliamua kuiweka hadharani?


Jike Shupa: Habari yangu ni nzuri. Kuhusu picha niliamua kuiweka mwenyewe na wala haina tatizo.

Ijumaa Wikienda: Unasema haina shida, lakini mjadala unaoendelea mtandaoni ni kwamba wewe ni mgonjwa sijui wa…

Jike Shupa: Sasa watu wameona tu hilo, kuna jambo kubwa zaidi ya picha hiyo. Hiyo picha ni trela. Ujumbe wangu ni kwamba wote waliotembea na mimi wakapime maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Ijumaa Wikienda: Kwa kauli hiyo unamaanisha nini?



Jike Shupa Namaanisha kwamba si hawa watu wanaishangaa hiyo picha yenye vipele na makovu? Nataka wote waliokuwa na waliotembea na mimi wakapime Ukimwi.

Ijumaa Wikienda: Lakini umeyachukualiaje maoni ya watu ya mtandaoni, hasa kuhusu suala la kujidhalilisha?

Jike Shupa: Sioni tatizo.

Wakati mwandishi wa habari hii anazungumza naye, Jike Shupa hakuonekana kuwa mgonjwa, ila mwili wake uliojaa vipele na makovu ulionekana dhahiri maeneo ya mikononi na miguuni.


KUMBUKUMBU

Mbali na picha hiyo ya wiki iliyopita, Jike Shupa amewahi pia kutupia picha nyingine ya akiwa ameanika ‘ikulu’ yake hadharani lakini kama hiyo haitoshi, amekuwa akinaswa kwenye matukio maovu likiwemo lile la kudaiwa kuwauza mastaa wenzake.

STORI: Imelda Mtema, DAR

Top Post Ad

Below Post Ad