Jokate: Ali Kiba Ndiyo Nani?


Jokate Julai 26.2018 alitia timu katika arobaini ya mtoto wa mtangazaji Zamaradi Mketema ilipofanyika nyumbani kwake Bunju, jijini Dar es Salaam.

Alipoingia tu, watu waliohudhuria katika arobaini hiyo waligeuka kumuangalia kama wamepatwa na mshangao huenda kwa kitendo chake cha kupotea kwa kipindi kirefu machoni mwa watu.

MCL Digital ilimtafa alipokaa na kuzungumza naye mambo machache juu ya ukimya wake, ilianza na swali la kutoonekana mitandaoni tu baada ya Mwanamuziki Ali Kiba kufunga ndoa.

"Noooo sitaki utaje jina la Ali Kiba, ukitaka tuzungumze uliza kitu bila kuweka hilo jina na nikwambie tu mimi sijakimbia mitandaoni nipo sana, sema watu wanashindwa kuniona sababu mara nyingi nakuwa nacomment kwenye kurusa za watu haswaa nikiona kitu kimenivutia

"Kitu kingine ni ubize na majukumu yangu, ndio yanayoniweka kimya kwenye masuala mengine," alisema Jokate

Jokate ambaye kimuonekano ukimuangalia amenenepa na kuzidi kunawili, ila ule ujauzito aliokuwa anadaiwa anao, hakuna hata dalili ya kuonekana.

MCL Digital iliendelea kumuuliza habari za madai ya kuwa na ujauzito, Jokate mitandaoni kuna mambo mengi acha na hilo swali.

"Hayo mambo ya mitandaoni ungeyaacha tu, hilo swali hapana kwangu"

Aidha Jokate amesena kila kinachoongelewa mitandaoni anavisoma na kuvipotezea kwani amegundua wapo watu hawajui matumuzi ya mitandao wanatakiwa wapate elimu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad