JPM Amteua Phaustine Kasike Kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza

Rais John Magufuli amemteua Naibu Kamishna wa Magereza, Phaustine Kasike kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza kuanzia leo Jumatatu Julai 13, 2018.

Taarifa iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema Kamishna Jenerali Kasike amechukua nafasi ya aliyekuwa Kamishna wa Magereza, Juma Malewa ambaye amestaafu.

Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Jenerali Kasike alikuwa Mkuu wa Chuo cha Urekebishaji Tanzania (TCTA) Ukonga Dar es Salaam.

Julai 6, 2018 Lugola alimfukuza kikaoni Malewa kwa kosa la kuchelewa katika kikao cha kimkakati cha viongozi wa taasisi za wizara hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad