Msanii maarufu wa muziki duniani, Justin Bieber amemvisha pete ya uchumba mchumba wake, Hailey Baldwin hii ni kwa mujibu wa mitandao ya habari za burudani nchini Marekani.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mtandao wa TMZ, zimeeleza kuwa Bieber alimvisha pete mchumba wake huyo siku ya Jumamosi iliyopita.
Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa wawili hao walivishana pete hiyo nchini Bahamas na kwenye tukio hilo hakuna mtu yeyote aliyeruhusiwa kurekodi kwa njia ya simu.
Baba yake na mrembo Baldwin kupitia ukurasa wake alithibitisha taarifa hizo lakini baadae muda mfupi alifuta Tweet.
Mama yake Justin Bieber pia naye aliandika kitu kwenye ukurasa wake wa Twitter kuashiria kuwa kuna jambo limetendeka usiku wa Jumamosi.